MARATTO

article · Eastern Africa Journal of Kiswahili (EAJK)

Mchango wa Fasihi ya Watoto katika Uwasilishaji wa Hisia

2026Open accessKaratina University

Abstract

Makala hii ililenga kubainisha jinsi hisia za watoto zinavyowasilishwa katika fasihi ya watoto ya Kiswahili, kwa kuzingatia mchango wa mazingira ya kifamilia na kijamii katika kuathiri hisia hizo. Fasihi ya watoto ni nyenzo muhimu ya kuakisi hali halisi ya maisha ya watoto. Hususan hisia wanazopitia katika mazingira yao ya kifamilia na kijamii. Mtazamo wa awali ulichukulia fasihi ya watoto kama chombo cha burudani na ufundishaji wa lugha. Fasihi ya kisasa inawakilisha kwa upana ulimwengu wa mtoto. Fasihi inaweka wazi changamoto, uzoefu na hisia mbalimbali katika maisha ya watoto. Kuna haja ya kuchunguza hisia zinazotokana na mazingira ya familia. Makala haya yalilenga kutathmini jinsi hisia za watoto zilivyowasilishwa katika fasihi ya watoto ya Kiswahili. Uchambuzi uliongozwa na Nadharia ya Uhalisia, ambayo ilisisitiza uwasilishaji wa maisha jinsi yalivyokuwa bila kupiga chuku. Kupitia nadharia hiyo, ilibainika kuwa waandishi waliwasawiri watoto wakipitia hisia kama vile furaha, huzuni, hofu, hasira, upweke, upendo na wasiwasi. Hisia hizo zilichochewa na mazingira ya kifamilia, uhusiano na wazazi, hali ya kiuchumi, migogoro ya ndoa, mazingira ya shule na mwingiliano wao na jamii. Utafiti huu ulitumia mbinu ya kimaelezo na uchanganuzi wa matini. Data ilikusanywa kutoka kwa novela zifuatazo: Ahaa! Roda, Mshale wa Matumaini na Siri ya Baba Yangu. Novela hizi ziliteuliwa kimakusudi. Uchambuzi ulionyesha kuwa familia ni mazingira muhimu katika kujenga na kuathiri ustawi wa kihisia wa watoto. Makala haya yalihitimisha kuwa fasihi ya watoto ya kisasa imechangia kuhalalisha hisia za watoto. Fasihi inaelimisha watoto kuhusu hali zao za kisaikolojia. Kwa msingi huo, makala haya yalipendekeza kuwa hisia za watoto zitambuliwe na zipewe uzito katika familia, shule na jamii ili kuimarisha ustawi wao wa kihisia, kijamii na kisaikolojia.

Research topics

  • Education and Vocational Training
  • Linguistic, Cultural, and Literary Studies
  • Literary Theory and Cultural Hermeneutics

Sustainable Development Goals

Read the original research

This page summarises published work. The authoritative version sits with the publisher.

DOI: 10.51317/eajk.v5i1.1132

Is something wrong with this record? Report it or request removal.

Discussion

Discuss this research

Have you built on this work, tried to replicate it, or seen it applied in practice? Share what you know. Verified researchers and MARATTO™ domain experts can open a discussion, and any member can reply. Contributions are reviewed before they appear.

No discussion yet. Open the first thread.